Saturday, October 3, 2009

mambo ndo hayo!!!!!bongo inatasha kimataifa

tanzania imedhiri kuwa ubora si lazima teknolojia ya juu,hii ndiyo spirit ya watanzania,kamwe haturudi nyuma kwa sababu mbazo hazina ukweli,hii ndo sababu inayonifanya kujivuna,wewe vipi?proud?let me know,soma utoe maoni
Korosho za Tanzania zimeshika nafasi ya kwanza kwa ubora katika soko la Dunia katika kipindi cha mwaka jana, imefahamika.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho nchini, Athumani Muhagama katika kikao cha kupanda dira ya bei ya zao hilo kwa msimu ujao.
Alisema ubora huo ulitokana na korosho hizo kupangwa kwenye madaraja kama wakulima walivyoshauriwa na wataalamu wa kilimo hicho na masoko ili waweze kuuza kwa bei nzuri.
Mkurugenzi huyo, alisema kwa sasa wakulima hao wana changamoto ya kuendelea kuboresha kilimo hicho na kuzingatia ushauri wa wataalamu ili zao hilo lizidi kuongoza mwaka hadi mwaka kwa ubora katika soko hilo.
Akizungumzia kuhusu mwaka juzi, alisema zao hilo halikufanya vizuri katika soko hilo kutokana na wakulima kuchanganya na takataka kwa lengo la kuongeza uzito.
Akifungua mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Magalula Said Magalula, alisema uwezo mdogo wa baadhi ya viwanda nchini wa kubangulia korosho nchini ni chanzo cha wakulima kulazimika kuuza korosho ghafi nje ya nchi, imeelezwa.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya wakati akifungua kikao kidogo cha Bodi ya Korosho cha upangaji bei kilichofanyika Ukumbi wa Andrew Kagwa mjini hapa. Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Said Meck Sadiki, Magalula, alisema licha ya kujitokeza matatizo hayo na ya kuyumba kwa soko la Dunia, uboreshaji wa kilimo cha korosho nchini ni muhimu kwa manufaa ya mkulima kwa kuuza zao hilo kwa bei nzuri na kuwa na uhakika wa soko.
Mgalula aliwaambia wajumbe wa kikao hicho kuwa kukata tamaa kwa wakulima kumesababisha mashamba mengi ya mikorosho kuachwa bila ya kusafishwa hali inayosabisha kuzaliwa magonjwa ambayo ni chimbuko la usumbufu wa zao hilo nchini.
Alisema kuwapo kwa magonjwa kwenye mikorosho kunawafanya baadhi ya wakulima ambao bado hawajakata tamaa ya kilimo hicho kutumia madawa mengi katika kukabiliana nayo.
Magalula, alisema kuwepo kwa matumizi makubwa ya madawa katika kilimo hicho kunamuongezea gharama mkulima na kumpunguzia faida na kwa mazingira hayo ndiyo yanayomlazimisha kuendelea kudai nyongeza ya bei kila mwaka.
Alisema endapo wadau wa kilimo hicho watajipanga upya kinaweza kuwa na faida kwa wote na kuongeza pato la Serikali. Katika kikao hicho wadau wamekubaliana dira ya bei iwe Sh 675 kwa korosho ya daraja la kwanza kwa kilo na Sh 580 kwa daraja la pili.
bongo inaweza,na ninaamini iko siku tutafika,hongera bongo na wakulima hawa wanaonyesha mfano,unaofaa kuigwa.toa maoni.

No comments: