Tuesday, December 8, 2009

Polisi wawakabili raia kwa risasi

Polisi wilayani Rorya mkoa wa Mara, wamefyatua risasi za moto katikati ya raia na kuua watu wawili na kuwajeruhi wengine tisa. Idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwani wakati tunakwenda mitamboni habari zilionyesha kwamba baadhi ya majeruhi walikuwa na hali mbaya.
Waliokufa katika tukio hilo, wamejulikana kuwa ni Iranda Matoka (26) na Abbas Adek (23). 
Aidha, majeruhi walitajwa kwa majina ya Wandiba Nyamkondya (26), Julius Nduku (26), Aziz Mganga (18), Sanga Matiko (32), Isiro Magesa (38), Ezekiel Robert (15), Ramadhani Magige (32), Musoba Rhobhi (32) na Leonard Kahanga.
Tukio hilo lilitokea jana, wakati askari hao walipokabiliana na wakazi wa kijiji cha Moharango, walioandamana kwenda kituo cha polisi Utegi, wakitaka kuachiwa huru kwa wazee wanne wa mila.

Wazee hao waliojulikana kwa majina ya Kahanga Mwando, Odila Runyola, Saba Kahanga na Wasaga Mganga, walikamatwa kwa madai ya kutishia kumroga na kumuua mkazi wa kijiji hicho, Joseph Ngondi.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa Nipashe, madai ya kumroga na kumuua Ngondi, yalitokana na hatua ya mwanakijiji huyo kufyeka mlima Nyabigiga, unaosadikiwa kutumika kwa masuala ya tambiko.

Watu walioshuhudia tukio hilo, waliliambia Nipashe kuwa baada ya wazee hao kukamatwa na kuwekwa ndani juzi, wanakijiji hao waliandama kwenda kituoni hapo kwa lengo linalodhaniwa kushinikiza kuachiwa kwa wazee wa kijiji, ndipo walipokabiliana na polisi waliokuwa na silaha zenye risasi za moto.
``Tulisikia milio ya risasi na baadaye vilio huku watu wakikimbia hovyo,`` mmoja wa mashuhuda ambaye jina lake halikupatikana, alisema.
Miili ya watu waliokufa na majeruhi ilipelekwa katika hospitali ya wilaya ya Tarime.

Majeruhi katika tukio hilo, miongoni mwao wakiwa katika hali mbaya, walijeruhiwa mikononi, miguuni, mgongoni na mapajani. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Liberatus Barlow, hakupatikana jana kuzungumzia tukio hilo.
 "hawa vipi jamani? unayaamini haya wanayoyafanya?toa maoni yako".

Wednesday, November 18, 2009

Chuo Kikuu IMTU chasitisha masomo ya udaktari wa meno

Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Udaktari na Teknolojia (IMTU), kimesitisha utoaji wa shahada ya udaktari wa meno (DDS) katika kipindi kisichojulikana kuanzia mwaka uliopita.


Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Joseph Shija, amewaambia waandishi wa habari kuwa masomo hayo yalisimamishwa tangu mwaka uliopita, ikiwa ni baada ya mabadiliko ya uongozi wa kitaaluma chuoni hapo.

Aidha, akasema kusimamishwa kwa shahada hiyo kunatokana na gharama za uendeshaji wa masomo hayo kuwa kubwa, idadi ndogo ya wadahiliwa na kuwepo kwa mhadhiri mmoja pekee chuoni hapo .

“Baada ya kuingia kwa uongozi mpya wa kitaaluma, tulifanya marekebisho ya uendeshaji na kuamua kusimamisha kwanza shahada ya madaktari wa meno,” akasema Profesa Shija.

Akasema ulipoingia uongozi mpya ulikuta wanafunzi walioomba kudahiliwa katika kozi hiyo ni 10 pekee, idadi ambayo ni ndogo kulinganisha na gharama za uendeshaji wa masomo katika fani hiyo.

Katika hatua nyingine, amesema idadi ya wadahiliwa katika chuo hicho imeongezeka kutoka jumla ya wadahiliwa 500 katika kipindi cha mwaka juzi hadi kufikia 900 Oktoba mwaka huu.

Akasema mafanikio hayo yametokana na uongozi mpya wa kitaaluma uliochukua nafasi za uongozi mwaka jana ambapo mchakato wa uendeshaji wa chuo hicho ulifanyiwa marekebisho.

“Awali katika masomo ya udaktari wanafunzi walikuwa wakisoma kwa muda wa miaka minne na nusu... lakini baada ya kuja kwa uongozi mpya, tumebadilisha na kuwa miaka mitano na hivyo kuendana na vyuo vingine vya udaktari ulimwenguni,” akasema.

Akasema kati ya wanafunzi hao waliodahiliwa, kumekuwa na ongezeko kubwa la wanafunzi wa Kitanzania tofauti na miaka ya nyuma ambapo Watanzania walikuwa hawazidi watano.

Akitoa mfano, akasema mwaka jana pekee, Watanzania waliohitimu walikuwa ni wawili , ilhali idadi kubwa ikibakia kuwa ya raia wa India ambao baada ya kumaliza masomo yao chuoni hapo, walirudi kufanya kazi nchini kwao India.

Akasema tangu uongozi huo uanze kazi mwanzoni mwa mwaka jana, idadi ya wadahiliwa imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka.

Tuesday, November 3, 2009

hii sheria vipi?Auawa Dar kwa tuhuma za wizi

Mtu mmoja anayedhaniwa kuwa ni kibaka ameuawa kwa kupigwa kwa mawe na wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa kukutwa akiezua mabati katika nyumba iliyokuwa ikiendelea kujengwa.

Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Mark Kalunguyeye amesema tukio hilo limetokea jana saa 3:30 usiku Kimara Stop Over , Jijini Dar es Salaam.
Akasema marehemu akiwa na wenzake watatu walifika katika nyumba hiyo inayomilikiwa na Bathelomeo Kijazi na kuanza kuezua mabati hayo kwa lengo la kuyaiba.
Hata hivyo, akasema wakati wakiendelea na uezuaji huo, majirani walisikia na kuanza kupiga kelele zilizowashtua watu wengine na kuanza kuwafuatilia.
“Waliposikia kelele, vibaka hao waliamua kushuka huku kila mmoja akabeba bati lake na kuanza kukimbia,”akasema.
Akasema wananchi walianza kuwafukuza na kufanikiwa kumkamata kibaka mmoja.
Kamanda huyo akasema baada ya kumkamata wananchi hao walimshambulia kwa mawe ambapo jiwe moja lilimpata kisogoni na kudondoka chini.
Akasema mtu huyo alifariki dunia wakati akipelekwa Hospitali ya Mwananyamala kwa ajili ya matibabu.
Akasema katika tukio hilo vibaka hao walifanikiwa kuondoka na mabati matatu na kuongeza uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea kuwakamata vibaka waliokimbia,
mambo vipi haya?toa maoni!!!!

Thursday, October 29, 2009

ulipuaji bomu wauwa dar

Watu wawili wamezirai baada ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) jana kufanya zoezi la kulipua mabomu katika kambi yake iliyopo Mbagala jijini Dar es Salaam.

Waliozirai katika tukio hilo la ulipuaji mabomu ni Rosemary Tarimo na aliyetambulika kwa jina la Matilda, ambao walikimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
Uamuzi wa Jeshi hilo kulipua mabomu yake unatokana na silaha hizo kulipuka zenyewe katika kambi ya Mbagala na kusababisha watu zaidi ya 20 katika eneo hilo kufariki dunia.
Zoezi hilo lilifanyika jana kuanzia saa 9:00 alasiri hadi saa 11:00 jioni ambapo kabla ya kufanya shughuli hiyo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Husein Mwinyi alitoa tahadhari kwa wananchi kukaa mbali wakati ulipuaji huo ukifanyika.
Akizungumza katika tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi alisema, licha ya taarifa kutolewa mapema kwa vyombo vya habari, ulipuaji wa mabomu hayo ulisababisha shughuli mbalimbali kusimama ikiwemo watu kufunga maduka yao na wengine kuhama nyumba kwa kuhofia kupoteza maisha yao.
Lukuvi alisema shughuli za ugawaji wa chakula katika kambi maalumu iliyojengwa kwa ajili ya kuwahifadhi watu walioathiriwa na mabomu yaliyolipuka yenyewe hivi karibuni nao ulisimama.
Aidha, Lukuvi alisema shughuli za kutathmini uharibifu wa mali uliotokana na mabomu hayo haujakamilika kutokana na ukosefu wa watalaamu kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.
Aliwaomba watu wenye ujuzi wa kufanya tathmini ya uharibifu wa mali kujitokeza haraka ili waweze kusaidia kujua thamani halisi.
Vilevile, Mkuu huyo wa mkoa alisema watu 14 bado wamelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na kuathiriwa na mabomu hayo yaliyolipuka huko Mbagala hivi karibuni.
Alisema mmoja wa watu hao hali yake ni mbaya na amelazwa chumba cha watu mahututi (ICU) katika hopitali hiyo.
Baada ya kutokea ajali hiyo watu mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara walianza kumimina misaada kwa wahanga ili kuwawezesha kujikimu baada ya baadhi yao kupoteza mali zao zikiwemo nyumba.
Zoezi la ilipuaji mabomu hayo jana lilishuhudiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali, Davis Mwamunyange.
"nibudi wananchi kulindwa na majanga yanayoweza kuepukwa".

Thursday, October 22, 2009

RAGE BADO YUMO!!!!! Simba wamtaka Rage kutowabeep

Wanachama wa klabu ya Simba wamemtaka Katibu Mkuu wa zamani wa Chama cha Soka Tanzaniai, FAT (sasa TFF), Ismail Aden Rage, aliyetangaza nia ya kuwania uenyekiti katika klabu hiyo 'kutowa-beep' bali agombee kweli.

Pia wanachama hao, wamesema wapo tayari kumpa nafasi hiyo Rage kutokana na wasifu wake katika soka na hususani klabu yao na hivyo wanamtaka ajitose kweli na sio kutishia toto tu.
Wakizungumza na Nipashe jana, baadhi ya wanachama hao, wakiwemo wazee walisema wamefurahishwa na taarifa kwamba Rage anataka kujitosa kwenye kinyang;anyiro cha uchaguzi mkuu ujao wa Simba, ila hawana hakika.
Mmoja wa wanachama na wazee wa klabu hiyo, Mzee Juma Hulungu, alisema kama ni kweli Rage ana nia ya kuwania uongozi Simba wanamkaribisha na kumhakikishia kuwa wanachama watampa nafasi atakayoiomba.
Hulungu, alisema hakuna wanachama wa Simba asiyemjua Rage na utendaji wake makini na jinsi alivyoisaidia mno klabu yao na hivyo ni muhimu ajitose ili wampe nafasi hiyo kuwaletea mafanikio na maendeleo.

Mwanachama mwingine 'kigogo' alisema kwa ufupi kwamba, kama ni kweli Rage anataka nafasi hiyo ajitokeze na wala asiwatie hamu wanachama kwani klabu yao inahitaji watu kama wao katika kuikwamua kimaendeleo.
Asitubeep, kama kweli anataitaka nafasi hii ajitokeze na hatutamuangusha, kwani tunathamini mchango na utendaji wake katika soka," alisema 'kigogo' huyo ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini.

Rage ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoa wa Tabora, alinukuliwa wiki iliyopita akisema ana dhamira ya kuwania Uenyekiti katika uchaguzi mkuu wa Simba utakaofanyika Desemba mwaka huu.

Kiongozi huyo anakuwa ni wa pili kutangaza kuwania nafasi hiyo, kwani tayari mwanachama mwingine wa Simba, Bossy Matola alishatangaza dhamira ya kurithi nafasi hiyo inayoshikiliwa na Hassani Dalali.

Wednesday, October 21, 2009

washa moto kikwete"wabongo tunakuaminia"

Kuna taarifa kuwa baadhi ya vigogo Serikalini wameanza kujawa hofu na kuhaha huku na huko kutokana na hofu ya kupigwa chini na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete, chanzo kikidaiwa kuwa ni fagio lake aliloanza kulipitisha kiaina katika kila eneo.

Aidha, hofu ya baadhi ya vigogo hao inadaiwa kutiwa nguvu na tetesi kuwa Rais anaendelea kuwang'oa kiujanja wale wote wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali yaliyoligharimu taifa.
Hadi sasa kuna mchakato wa kuisafisha Serikali kwa kuwawajibisha wale ambao utendaji kazi wao hauridhishi na pia wale wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali, chanzo kimoja kutoka Serikalini kimesema.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, baada ya taarifa ya Rais kufanya mabadiliko katika safu ya Makatibu Wakuu na kuteua Mwanasheria mpya wa Serikali juzi na jana, hali imeendeea kuwa tete kwenye baadhi ya ofisi.
"Haya mabadiliko yaliyotangazwa juzi na jana yamekuwa tishio kwa baadhi ya vigogo... wengine wameanza kuhaha kutokana na hofu kuwa pengine nao watakumbwa na fagio la kuwatema kwa sababu mbalimbali," kikadai chanzo hicho.
Aidha, kikaongeza kuwa hivi sasa, baadhi ya vigogo wamekuwa hawatulii maofisini kwani muda mwingi wamekuwa wakinusanusa taarifa toka Ikulu juu ya kusikia kama kuna badiliko lolote.
Juzi, Rais Kikwete alifanya mabadiliko ya makatibu wakuu wa baadhi ya Wizara, ambapo wengine waliachia ngazi kutokana na maelezo kuwa muda wao wa kusitaafu kwa lazima umewadia ilhali wengine wakihamishwa toka wizara moja hadi nyingine.
Aidha, jana Rais Kikwete alimteua Jaji Fredirick Mwita Werema kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, akichukua nafasi ya Johnson Mwanyika ambaye anastaafu.
Hata hivyo, Mwanyika ni miongoni mwa vigogo ambao Bunge lilitaka wawajibishwe kwa tuhuma za kuhusika kwao na kashfa ya kampuni tata ya umeme ya Richmond, kama ilivyo kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi, ambaye naye ameondolewa nafasi hiyo na Rais kwa maelezo kuwa anakwenda likizo ya kustaafu.

Sunday, October 18, 2009

wabongo pia ni wacheshi!!!!!!!!!

Bongo kuna kina Mr Bean weengi 'Wachekeshaji' lakini kila mtu ana style yake ya uchekeshaji, huyu ye anakwambia anauwezo wa kuchekesha Ki Mr Bean vitendo bila kuongea na anaweza kwa vitendo na kulonga.
Ukipata nafasi ya kukaa na Mkwele dakika chache na kupiga naye stori unaweza kujiuliza hivi familia yake inaishi vipi naye? Si wanacheka kila saa?
Kijana huyo ana kila sifa anayotakiwa kuwa nayo mchekeshaji. Unapozungumza naye ana maneno mengi ya kuchekesha, ambayo muda wote utajikuta ukifurahi kumskiliza na kuangua kicheko.
Anaweza akakuangalia asizungumze lolote ukajikuta ukicheka tu kutokana na vitimbi vyake na jinsi anavyojibaraguza na kugeuzageuza macho na mdomo.
Mkwele ambaye ni nadhifu mno anapokuwa mitaani, anasema anaweza kuigiza vizuri zaidi vichekesho kuliko filamu.
Anasema katika filamu huwa hajisikii huru wala haoni kama anaziweza 'kufoji' au kujilazimisha. "Unajua kipaji changu mimi ni kuchekesha ndio maana mara nyingi unaniona nafanya komedi na ndio zilizoniweka kwenye chati kuliko filamu au maigizo mengine ya kawaida,"anasema.
"Komedi naimudu na naiweza kwani pamoja na kuigiza nina uwezo mkubwa wa kuitengeneza sura yangu na kuonekana kichekesho bila hata ya kuongea lolote.
"Fani ya uigizaji hasa ya komedi ni ngumu sana tofauti na watu wengine wanavyofikiria, inahitaji ubunifu wa hali ya juu ili kuikamata hadhira,"anasema Mkwele.
"Uigizaji wa kawaida pamoja na kuwa una ugumu lakini ni rahisi kwani utakapotakiwa uigize kama Baba, Hakimu, Mama mtu yeyote anaweza kufanya hivyo ilimradi awe na kipaji cha kuigiza tu.
"Lakini linapokuja suala la kuchekesha ni kipaji cha ziada usifanye masihara kubuni kitu kumfanya mtu acheke si kazi ndogo hata kidogo, ni kweli kabisa nimeshiriki katika filamu kama 'Cleopatra' na nyingine mbili lakini sioni kama ninafanya vizuri kama ninavyofanya kwenye Mizengwe."
"Unajua katika maisha, pamoja na kuwa kila mmoja wetu ana fani yake wakati mwingine si vibaya kujaribu kazi nyingine hasa katika kujitafutia riziki," anasema.
Akizungumzia wasanii anaowazimikia ndani na nje ya nchi Mkwele anasema wa ndani ni Binti Kiroboto na wasaanii wa nje ni Harrison Ford na Mr. Bean.
"Uchekeshaji kimataifa umekuwa na soko sana tofauti na hapa kwetu na hii ni kutokana na Watanzania wengi kutopenda kuthamini kazi za wenzao jambo linalotufanya tudumae.
"Lakini mipango yangu ya baadaye ni kuhakikisha kazi zangu zinafahamika kitaifa na kimataifa, si hivyo tu pia nimedhamiria kufanya kazi kwa bidii ili hadi kufikia mwaka 2012 panapo majaaliwa nianzishe kitu changu, inaweza kuwa kampuni studio au kitu chochote."anasema
Mkwele na kutoa wito kwa wasanii wote nchini waichukulia fani hiyo kama kazi na kuifanya kwa kujali miiko. "Kwa kufanya hivyo sanaa itafika mbali hata kama hatutawafikia kina Rambo lakini tutawakaribia."
"Ili ndoto za wasanii zifanikiwe serikali ina kazi kubwa ya kuwalinda wasanii kwa kutunga na kusimamia sheria zinazoangalia kazi za wasanii nchini," anasema.
Kuhusu uhusiano wa kimapenzi, Mkwele anasema ana mchumba na mtoto mmoja ingawa hakutaka kuzungumzia kiundani zaidi kwamba dada huyo ni yupi.
"Bado nazichanga ili nifunge ndoa na mchumba wangu, si unajua tena maisha yalivyoba kwa sasa?"anasema mchekeshaji huyo ambaye amekuwa kwenye chati hasa katika kikundi cha Mizengwe kinachorushwa na kituo cha televisheni ya ITV.
mambo safi bongo au siyo.hongera.

Saturday, October 17, 2009

Watanzania wawili 'waula' taasisi za kimataifa

JAJI Bernad Luanda pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC), Godwin Ndossia wamechaguliwa kufanya kazi katika taasisi mbili tofauti za kimataifa.


Wakati Jaji Luanda amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa chama cha majaji na mahakimu wa Jumuiya ya Madola kanda za Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na Kusini ya Afrika, Ndossi amechaguliwa kuwa mwakilishi wa Bara la Afrika kwenye kamati ya utendaji ya Shirikisho la Kimataifa linalojishughulisha na Sayansi ya Lishe Duniani (IUNS).

Jaji Luanda alichaguliwa hivi karibuni katika uchaguzi uliofanyika katika kongamano la mkutano mkuu wa majaji ulioketi katika visiwa vya Turks na Caicos vilivyopo Caribbean.

Taarifa iliyotolewa na Msajili wa Mahakama ya Rufaa nchini, Francis Mutungi, ilisema kongamano hilo liliwachagua pia Jaji Norma Wade Miller kutoka Bermuda (Kanda ya Caribbean ) kuwa Rais wa chama hicho.

Jaji Luanda ni Rais wa chama cha majaji na mahakimu cha Tanzania, pia makamu wa kwanza wa Rais wa chama cha majaji na mahakimu cha Afrika ya Mashariki.

Ndossi yeye alichaguliwa kwenye nafasihiyo katika mkutano wa IUNS uliofanyika kuanzia Oktoba 4 hadi 9, mwaka huu nchini Thailand.

Akizungumzia jijini Dar es Salaam juzi, Ndossi alisema ni mara ya kwanza kwa Mtanzania kuteuliwa kwenye nafasi ya kuwakilisha bara la Afrika katika taasisi hiyo nyeti ya IUNS ambayo hujadili masuala muhimu ya lishe duniani.

Lakini akasema ni changamoto kubwa kwake hasa katika kipindi hiki ambacho dunia inakabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamesababisha ukame ambao umedumu kwa miaka miwili.

"Hali ya lishe kwa bara la Afrika ni mbaya sana. Ukame umaathiri uzalishaji wa chakula na kasi ya utapia mlo inaongezeka kwa kasi kubwa," alisema Ndossi.

Katika bara la Afrika, alisema nchi zinazokabiliwa na utapiamlo wa kutisha ni zile ambazo zinakabiliwa na machafuko ya muda mrefu ya vita kama vile Somalia na Sudan.

Utafiti uliofanywa na TFNC siku za karibuni, Ndossi alisema unaonyesha kwamba wilaya za Longodo mkoani Arusha na Nachingwea mkoani Mtwara, ndizo zilizokatika hali mbaya ya utapia mlo hapa nchini.

Katika utafiti huo ambao alisema unatarajia kutolewa na TFNC karibuni, wilaya nyingine ambazo nazo zinakabiliwa na tatizo hilo nchini pamoja na mikoa ilipo kwenye mabano ni Bagamoyo (Pwani), Same (Kilimanjaro), Ruangwa (Lindi), Kongwa (Dodoma), Monduli (Arusha) na Mufindi (Iringa).

Akielezea juu ya hali hiyo ya utapia mlo, Ndossi alisema wanawake na watoto ndio wanataabika kwa kiwango kikubwa na tatizo hilo.

Kuhusu vigezo vilivyotumika katika kupima tatizo hilo alisema: "Tulichunguza hali za afya za kinamama na watoto. Katika jamii hawa ni kama pima joto ya tatizo la utapiamlo," alisema mjumbe huyo wa Afrika IUNS.

mambo si ndo hayoo!!!je wabongo mnasemaje?sema maoni yako.

Saturday, October 3, 2009

mambo ndo hayo!!!!!bongo inatasha kimataifa

tanzania imedhiri kuwa ubora si lazima teknolojia ya juu,hii ndiyo spirit ya watanzania,kamwe haturudi nyuma kwa sababu mbazo hazina ukweli,hii ndo sababu inayonifanya kujivuna,wewe vipi?proud?let me know,soma utoe maoni
Korosho za Tanzania zimeshika nafasi ya kwanza kwa ubora katika soko la Dunia katika kipindi cha mwaka jana, imefahamika.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho nchini, Athumani Muhagama katika kikao cha kupanda dira ya bei ya zao hilo kwa msimu ujao.
Alisema ubora huo ulitokana na korosho hizo kupangwa kwenye madaraja kama wakulima walivyoshauriwa na wataalamu wa kilimo hicho na masoko ili waweze kuuza kwa bei nzuri.
Mkurugenzi huyo, alisema kwa sasa wakulima hao wana changamoto ya kuendelea kuboresha kilimo hicho na kuzingatia ushauri wa wataalamu ili zao hilo lizidi kuongoza mwaka hadi mwaka kwa ubora katika soko hilo.
Akizungumzia kuhusu mwaka juzi, alisema zao hilo halikufanya vizuri katika soko hilo kutokana na wakulima kuchanganya na takataka kwa lengo la kuongeza uzito.
Akifungua mkutano huo, Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Magalula Said Magalula, alisema uwezo mdogo wa baadhi ya viwanda nchini wa kubangulia korosho nchini ni chanzo cha wakulima kulazimika kuuza korosho ghafi nje ya nchi, imeelezwa.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya wakati akifungua kikao kidogo cha Bodi ya Korosho cha upangaji bei kilichofanyika Ukumbi wa Andrew Kagwa mjini hapa. Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Said Meck Sadiki, Magalula, alisema licha ya kujitokeza matatizo hayo na ya kuyumba kwa soko la Dunia, uboreshaji wa kilimo cha korosho nchini ni muhimu kwa manufaa ya mkulima kwa kuuza zao hilo kwa bei nzuri na kuwa na uhakika wa soko.
Mgalula aliwaambia wajumbe wa kikao hicho kuwa kukata tamaa kwa wakulima kumesababisha mashamba mengi ya mikorosho kuachwa bila ya kusafishwa hali inayosabisha kuzaliwa magonjwa ambayo ni chimbuko la usumbufu wa zao hilo nchini.
Alisema kuwapo kwa magonjwa kwenye mikorosho kunawafanya baadhi ya wakulima ambao bado hawajakata tamaa ya kilimo hicho kutumia madawa mengi katika kukabiliana nayo.
Magalula, alisema kuwepo kwa matumizi makubwa ya madawa katika kilimo hicho kunamuongezea gharama mkulima na kumpunguzia faida na kwa mazingira hayo ndiyo yanayomlazimisha kuendelea kudai nyongeza ya bei kila mwaka.
Alisema endapo wadau wa kilimo hicho watajipanga upya kinaweza kuwa na faida kwa wote na kuongeza pato la Serikali. Katika kikao hicho wadau wamekubaliana dira ya bei iwe Sh 675 kwa korosho ya daraja la kwanza kwa kilo na Sh 580 kwa daraja la pili.
bongo inaweza,na ninaamini iko siku tutafika,hongera bongo na wakulima hawa wanaonyesha mfano,unaofaa kuigwa.toa maoni.

Monday, September 28, 2009

bongo yetu shwari
katika yote ninayoyafanya hakika moyo,fikra na matumaini yangu bongo iendelee kuwa shwari,hakika bongo haina mfano pamoja na yote ambayo unaweza fanikiwa katika nchi za nje,tusiwe wachoyo wa fadhila,au vipi?

ninaamini yakuwa bongo ni kati ya nchi ambazo zina nafasi kubwa za kimaendeleo,nikweli kuwa mshiko ni haba,nikweli kuwa nchi haina uchumi ulioboreka,

haya yote ni matokeo ya ukoloni,na kamwe tusije kuutumia uchumi ulio chini kama kisingizio,wote wameanza chini lakini hawakukata tamaa na sasa wanayavuna matunda.

watanzania tulio nje tunaweza,na wala hatuna kisingizio,tuisaidie nchi yetu,tuonyeshe umoja na tuendelee kufanya kazi kwa bidii,tufaham ni kipi kimetuleta humu,tutafute namna mbalimbali zitakazo tuwezesha kushiriki katika mambo mbalimbali yanayoihusu tanzania,nafaham kuwa nivigumu sisi kupata taarifa sahihi na mwongozo,lakini kwanza tuwe wamoja,tushauriane,na tuone yale ambayo tunaweza kuyafanya,

pia ninapatikana humu http://ngasmet.topoffers.us au http://ngasmettopoffers.blogspot.com

bongo mpya ya kikwete,incredible!!!

hakika chenye mwanzo kina mwisho na siasa za kizamani hazina mpango bongo,na msela ameliona hilo,au siyo?hongera bongo tuko pamoja,soma uniambie maoni yako,tuongee bongo kama kawa.

Mheshimiwa mkubwa wa nchi,Jakaya Mrisho Kikwete,Jumatano, Sep 9, 2009, alitoka na style mpya kabisa ya kuchonga moja kwa moja na wananchi kupitia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na vyombo vingine vya utangazaji nchini kuanzia saa mbili na nusu usiku.

Mbali na TBC, televisheni nyingine za ITV, TVZ, Mlimani TV, Tumaini TV na Channel Ten zilitarajia kuonyesha mazungumzo hayo.JK alitumia aina mpya ya kuwasiliana na wananchi kwa kusikiliza hoja zao, kwa kujibu maswali , kusikiliza ushauri wao na kupata maoni juu ya mambo yanayohusu mustakabali wa bongo.

JK pia alisikiliza matarajio ya wananchi katika jitihada zao za kuboresha maisha yao kwa kujiletea maendeleo.kuanzia saa 2:30 hadi 4:00 usiku

Aidha mazungumzo hayo yalitangazwa kwenye redio
TBC-Taifa,
Sauti ya Tanzania,
Zanzibar, Radio Mlimani,
Radio Clouds,
Radio Tumaini, na
Radio Uhuru.
ushauri ulipokelewa
"hii ni kweli au jamaa anatuzuga ili apate mradi wake"

madenti hawa vipi?

Masela watatu, akiwamo denti wa kidato cha sita katika Skonga ya Sekondari ya Azania, wamenaswa wakiwafanyia (paper) mitihani wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).Frank Kaduma, aliyekuwa anamfanyia mtihani mwanafunzi aliyemtaja kwa jina moja la Tina, alikuwa ameahidiwa na mtu aliyemuunganisha na mtahiniwa huyo kuwa baada ya kutoka kwenye mtihani huo angelipwa sh 150,000.


Kwa mujibu wa Msajili wa Wanafunzi chuoni hapo,kitambulisho alichokuwa akikitumia Frank kumfanyia Tina mtihani kilikuwa na jina la Christian Mbago, mwanafunzi wa mwaka wa tatu.Akijieleza mara baada ya kunaswa Frank alisema kuwa...aliitwa na rafiki yake ambaye hata hivyo hakutaka kumtaja jina, na baadaye alimuunganisha na mtahiniwa na kukubaliana kiasi hicho cha fedha baada ya kazi hiyo kumalizika.“Mimi ninasoma Azania, nachukua PCM (Fizikia, Kemia na Hisabati), rafiki yangu anasoma masomo ya biashara na mtihani wa leo una hisabati, hivyo juzi nilikuja naye ili anionyeshe darasa na leo ndiyo nimekuja kumfanyia mtihani,” alisema Kaduma.

Wakati mwanafunzi huyo akihojiwa, mwanafunzi mwingine, John Kapinga, alikamatwa na kupelekwa katika ofisi ya msajili baada ya kukutwa akimfanyia mtihani mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuoni hapo, Joel Mlengule, anayesoma Stashahada ya Juu ya Hifadhi ya Jamii (Advanced Diploma in Social Protection).

Kapinga, alikiri kuwa alihitimu kidato cha sita mwaka 2003, akisoma masomo ya PCM, pamoja na kuahidi kwamba angetoa ushirikiano ili kumkamata mtahiniwa halisi.“Sikutaka kufanya, ila nilishawishiwa mara nne sikutaka, hata ikafikia hatua ndugu yake kunishawishi, nikakubali, ila dhamiri ikinisuta. kwani hakuna malipo yoyote tuliyoahidiana na ndugu yangu huyo,” alisema Kapinga huku akijiinamia.Chanzo chetu kilishuhudia kitambulisho chake kikiwa na jina la Joel Mlengule, kikiwa na namba ya usajili ADSP/16492/2007 na kinamalizika muda wake mwaka huu.Kwa upande wake, Joel Mlengule, aliyefanyiwa mtihani na kukamatwa akiwa nje ya eneo la IFM akimsubiri Kapinga, alinaswa na walinzi wa chuo na kuhojiwa, ambapo alikiri kufanyiwa mtihani na Kapinga.

Mlengule ambaye ni mkazi wa Upanga, jijini Dar es Salaam, alikiri kuwapo mtu aliyemuunganisha na Kapinga, baada ya kufeli somo lake la hesabu mara mbili mfululizo, hivyo hakutaka hali hiyo imrudie, hasa ikizingatiwa kuwa huo ulikuwa mtihani wa mwisho chuoni hapo.“Ni kweli alikuwa ananifanyia mtihani baada ya kufeli somo hili mara mbili. Niliona mwaka huu, na huu ni mtihani wangu wa mwisho, mimi sijui hesabu, ndiyo maana hata aliponiambia anifundishe nilikataa na kumwomba anisaidie kunifanyia,” alisema Mlengule.

Kwa mujibu wa Msajili wa Wanafunzi chuoni hapo, tukio jingine la namna hiyo lilitokea hivi karibuni, ambapo msichana mmoja alikimbia na kuacha viatu vyake, baada ya kubainika kuwa alikuwa akimfanyia mtihani mwanafunzi ambaye jina lake halikupatikana mara moja.Aliongeza kuwa, mwaka jana matukio hayo yalitokea na imebainika kuwa kuna wakala anayewaunganisha wanafunzi wa chuo na watu wa nje kuwafanyia mitihani hiyo kinyume cha taratibu.
 
ninajiuliza tutafika kweli hivi?kwa kweli hii ni hatari kwa maendeleo ya nchi yetu,toa maoni yako by mwandishi.

bongo pia imo

tanzania ni kati ya nchi duniani zenye raslimali ya kujitosheleza,lakini ni nani anayefaidika nayo?asili mia kubwa ya rasilimali yetu bongo bado haijatumika bado na kiasi kilichogundulika,ni cha walami/wazungu,ukiuliza kwanini,utapewa sababu tele!!wewe ungelijibu vipi?




bongo inapasa kuwa na mipango endelevu ya kimaendeleo,yenye kufwatilia shughuli zote za uzalishaji,chukulia mfano madini ya tanzanite,hakika madini haya adim duniani hayana mipango madhubuti ya kitaifa,mwishowe uchimbaji holela ambao unapelekea kunufaisha nchi za nje na wananchi wao,sababu ni nini?watanzania hawana mitaji,hili ni jibu kweli?sina imani najibu hilo,mimi ninaamini,watanzania walio nje wangelishirikishwa nchi yetu ingenufaika.



kwakweli hili linasikitisha,mimi ninahofia hatima ya nchi yetu hapobaadae,na bado ninasisitiza tusiwe niwenye kujisahau na kusahau tulipotoka,tuisaidie nchi yetu,tanzania ndo sisi na sisi ndo tanzania,toa maoni ili niweze kuelewa unamawazo gani, visit http://ngasmet.topoffers.us or http://topoffers.blogspot.com for more.

Thursday, September 24, 2009

rasilimali yetu sisi wabongofrom watanzania marekani tuongee

rasilimali yetu sisi wabongofrom watanzania marekani tuongee


kilimanjaro ni kati ya milima mirefu na mashuhuri duniani,mlima huu ni kivutio kikubwa kwa watalii kutoka sehemu mbalimbali za dunia,



hizi zote zinapasa kuwa ni sababu tosha kabisa za kuulinda na kuhakikisha mlima huu unawafaidisha watanzania wote na hususan wale wa vijiji vya karibu na mlima huu wa kipekee.



ni matumaini yangu mimi na watanzania wote kuwa serekali itaendelea kuboresha sera na kanuni zinazohusian na matumizi ya mlima huu mrefu kuliko yote africa,



kwa hakika tusipoutunza kwa kuhakikisha,wapandaji hawayaaribu mazingira ya mlima,basi mlima huu wa kipekee utapoteza ubora wake na hatimae nchi itakuwa imepoteza chanzo muhimu kabisa cha mapato.



watanzania pia tunajukum la kuiunga serekali yetu mkono na kusaidia katika kuuboresha mlima huu na na mazingira yake,ili kuendelea kupata faida,na kuitumia raslimali hii kwa miaka mingi ijayo.andika maoni.